21/05/2013

Hadithi ! Rushwa imeanzishwa na... chiriku !Wanyama wale walikuwa wamepigiwa kura. Wakipigiwa kura na ndege wote hapo wa duniani, wakasema kwamba huyu Tondohore na Chiriku na Kikui, hao ndio wataoendesha nchi. Wanaweza kuiongoza lakini uraisi apewe nani ? Basi wapige kura. Ikakubalika lakini raisi awe Chiriku.
Sasa anakuja yule Mwewe au Pozi au Kimbanga, basi akimwona yule anakuja Chiriku anamwambia :
twara twara yo yo soro ya piri !
Kwa sababu yule anakuja kuchukua ndege wenzake ! lakini kwa kuwa ameshapewa rushwa :
- bwana nini ? chukua hela hii, nikija nikatie ndege nipate kula ! lakini nikija usiwaambia upesi mpaka nimchukue mmoja, yaani usiwashtue ! nikichukua mmoja au wawili... 
- sawa !
Anachukua hela anaweka. Kwa hivyo yule akifika tu, Chiriku anasema :
- twara twara yo yo soro ya piri !
Maana yake « chukue mmoja usichukue wawili ».
Kwa sababu Chiriku ana maneno yake :
- kawiwi saracha nsiyo mangara kagi kanononono ndogiyo kumi… ».
Kila siku anafanya vile, mpaka wanakwisha ndege. Ndege wakaanza kuomba mkutano, wakaweka mkutano :
- bwana wee ! mboni tunakwisha ? vipi ? 
Wakasema :
- tuanze kupiga kura, Chiriku hatufai ! »
Wakipiga kura :
- raisi awe nani ?...
- Tondohore ! (ndege mweusi mwenye kishungi, anakula sana matope).
Haya !
- makamo raisi tuweke nani ? 
- tumweke Kikui ! (mlio wake kama kapiga firimbi yule, hasa kama anamwona ndege anapita, tuseme Pozi, anapiga mluzi yule !)
Sasa pale sawa imekubalika, Tondohore raisi, lakini muda huo, kishungi hana kile ! na wala Kikui manyoya laini yale, hana. Ikabidi pale, yule Pozi anakuja. Akija anamwambia :
- bwana wewe nikupe rushwa ! 
Tondohore akasema :
- mimi sichukui rushwa !
Anakataa. Akajibu :
- ah ! kama hutaki kuchukua rushwa, basi mimi nitachukua nguvu, ndege wenzako nitachukua tu ! 
Akamwambia :
- sawa, lakini mimi rushwa sipokei na nitawashtua wale waondoke ».
Basi mpaka leo kama anakuja yule Pozi, akimwona yule Tondohore anasema :
- pwi pwi ! pwilikiti ! (mfano mlio wake twe twe !).
Basi hata kama kuku, wote wanajificha, ndege wote kimya jiii ! kwenye majani wanaingia, kwenye pori wote wanajificha. Sasa Tondohore akishafanya « pwilikiti ! », wote wameparanyika :
- ondokeni ! ».
Na yule Kikui akilia, Tondohore naye anafanya « piririririri... », wale wanapotea kabisa, na kama Tondohore hajaona, Kikui ana mlio huu, basi tayari vile vile ! Wote wakasema sasa hao wamekubalika :
- tufanye nini ? 
- Tondohore, tumpe kofia ambayo hata kama anakufa nayo, ndo akapewa kile kishungi.
- Kikui tumpe nini zawadi yake ? 
- tumpe nguo za hariri, laini mno za joto na baridi asiisikie ! »
Ndo maana nguo za Kikui laini ! kama sufu kwa jina lingine, safi kabisa ! anapendeza... maridadi mno. Na mpaka leo ni raisi ! nguo za shani, za murua !! Zamani ya kale, alikuwepo mshairi mmmoja aliyeitwa Aristophanes...

Samahani wapendwa wasomaji kwa kutaja hapa chini dondoo mojawapo la mwandishi mashuhuri kutoka Ugiriki, ambaye jina lake Aristophanes. Mshahiri huyu alizaliwa mnamo mwaka 450 au 445 kabla J.-K.  (Plato alizaliwa mwaka 424). Dondoo hilo limetoka katika tamthilia yake maarufu iitwayo « Ndege » inayojadilia kwa undani uwongo wa siasa, rushwa na maporojo ya kipuuzi wa viongozi wetu. La kustaajabu ni kwamba hadithi ile ya juu ambayo msimulizi wake alikuwa mzaliwa wa Kilwa (marehemu mzee Suleiman Mawi), inafanana sana na alichokusudia kuthibitisha Aristophanes !! Kwa kifaransa : 

La huppe, dans le taillis :

" Epopopopopopopopopopoï ! lo, lo ! Venez, venez, venez, venez, venez ici, ô mes compagnons ailés; vous qui paissez les sillons fertiles des laboureurs, tribus innombrables de mangeurs d'orge, famille des cueilleurs de graines, au vol rapide, au gosier mélodieux; vous qui, dans la plaine labourée, gazouillez, autour de la glèbe, cette chanson d'une voix légère : "Tio, tio, tio, tio, tio, tio, tio, tio;" et vous aussi qui dans les jardins, sous les feuillages du lierre, faites entendre vos accents; et vous qui, sur les montagnes, becquetez les olives sauvages et les arbouses, hâtez-vous de voler vers mes chansons - Trioto, trioto, totobrix ! - Et vous, vous encore qui, dans les vallons marécageux, dévorez les cousins à la trompe aiguë, qui habitez les terrains humides de rosée et les prairies aimables de Marathôn, francolin au plumage émaillé de mille couleurs, troupe d'alcyons volant sur les flots gonflés de la mer, venez apprendre la nouvelle. Nous rassemblons ici toutes les tribus des oiseaux au long cou. Un vieillard habile est venu, avec des idées neuves et de neuves entreprises. Venez tous à cette conférence, ici, ici, ici, ici. -Torotorotorotorotix. Kikkabau, kikkabau, torotorotorotorolilililix. "

- In Les oiseaux, Aristophane.Hakuna maoni:

Chapisha Maoni