15/09/2013

SULTANI AMEKULA BAKORA !

Ilani : kifuatacho ni hadithi simulizi. Sikuthubutu kuikosoa wala kuirekebisha kwa sababu moja kuu : hadithi husimuliwa kwa kutumia sauti, si fasihi andishi. Maongezi au simulizi si maandishi wala fasihi...


"Alitokea bwana mmoja, bwana huyu maskini. Maskini alikaa karibu na Sultani, jirani. Sultani ana watoto wake, ana vijakazi, ana watwana, kila mali. Sasa yule maskini hana chochote na watoto anao. Kazi yake porini kupita kutafuta asali ndio kwenda kula watoto wake. Watoto wake wale wanaenda kutumikia kwa Sultani kupata ukana ndo wanakula. Hana chochote na mkewe.

Sasa kazi yake hiyo imekwenda, kwenda zake porini akenda kuukuta mti mkubwa. Pale akafanya kivili kupumzika kwanza. Hajapata chochote na nyumbani watoto amewacha hivi hivi hawana kitu cha kula. Sasa kutoka pale alichukua shoka aliyochukua kupita kubangulia asali, akapiga kwenye mti ule, bom ! anasema : « ah! ah ! nani wewe unatuumiza ? » Katika mti unasema ndani : « unatuumiza wewe nani ? » Anasema : « mimi maskini bwana, sina kitu chochote hivi taharaki ya njaa nataka kurudi sina kitu ».

Basi pale, kwa swanaa zake kimetoka chano, wametoa chano wale waliokisema. Wakamtupia. Wakamwambia : « unatuumiza wenye mti ule, chano hicho uchukue, ukenda nyumbani useme chano andika, na kama unabisha mti wowote utapokaa, sema chano andika ! basi kila unachokitaka wewe faradhi humo hela humo, hela ya kutumia humo, mafuta kila kitu, utapata humu ».

Bwana yule kakichukua chano kile, akienda akatafuta mjiti mzuri mvili akakaa, njaa imemshika. « Nimeambiwa chano hiki kila kitu nikipate humo, mimi nina njaa nataka kula sasa. Wee chano andika ! » Kapewa sahani ya wali pale na mchuzi wake na maji yake hakuna kitu cha kutafuta. Akala tayari, akashiba huyu anachukua, vyombo vyake na chano chake.

Sasa anawakimbilia watoto wake nyumbani. Amekwenda mpaka nyumbani amewakuta wamelala ropoto, mama mtu ndo alio macho. « Nyinyi watoto ? », « njaa ! toka ule ule uliotoka wewe hakijapatikana chochote ». « Haya waamshe kwanza ». Akawaamsha : « amsha ! » Amewazungusha pale wote, akasema : « wee chano andika ! mimi watoto wangu hali zao hizi wanataka kula ». Kumeandikiwa pale sinia ya wali. Mchuzi na maji, kila kitu wala hatoki mtu kwenda kutafuta pale wanakula watoto, shibe shibe ! na mama mtu kimbele pale pamekwisha.

Baba mtu anaingia msalaani kwenda kukoga maji anavaa tena kamili mwanamme anapita kutembea. Pale anamwambia mkewe : « hiki chano weke chumbani, nataka taimu ya kula unachukua wewe unasema unapata kula hawa watoto na mwenyewe », « ndiyo ». Akiweka.

Siku lile, siku la pili, kule Sultani yule sasa anawauliza wale watwana wake wanamwambia : « maskini siku hizi hajaenda porini, watoto wake hapa hawajaja amepata msingi gani ? » Aliokaa nyumbani hivi wanasema : « hata hatuelewi, tunawaona, raha moja kwa moja, watoto wake, sasa wanene. Hata mtaji wake aliopata hatuujui ».

Sasa watoto wadogo sasa, kukutana na wale, wanasema : « nyinyi kwa nini siku hizi kwetu hamuji, imekuwaje mnakula nini ? » Wanasema : « ah ! baba kapata chano ! » Hivyo ndo wanaanza sasa. « Baba kapata chano, ndani humu ameweka mama, mama akisema chano andika basi tunakula mpaka tunaacha, wala hatuna njaa wala hatuna nini, hapa tulipo ».

Watoto wale wameyachukua kwa baba yao Sultani. Wanasema : « maskini siku hizi tajiri, amepata chano, chano hicho kila kitu unachokitaka humo, watoto wake wale ndo waliotuambia sisi ». Anawaambia : « ah ! nyinyi sasa kesho, chukueni safari, mchukua vyano hivi vilivyo ndani mukaambie twendeni kisimani tukaoshe vyano hivi tukakoshe kisimani. Basi mkienda huko, mkikosha, muwabadili chano hicho muchukue nyinyi muwape kingine. Ah ! nendeni, basi ».

Asubuhi wake watoto wamepanganyika mpaka pale. « Jamaani wee, sie tunakwenda kukosha vyano vyetu hivi kisimani, twendeni », « nasi tukachukue chetu ». Mama yao alikwenda kuzunguka wapi ? sijui, chumbani. Wakienda wakichukua : « chano hichi chano chetu twendeni tukaoshe ». Wakenda kule wanaosha wanafanyaje habari ya watoto : « hebu kwanza tutazame, hiki na hiki kizuri chepi ! », « hiki kizuri ». Wamewabadilishia wanawapa kisichoandika.

Wanarudi mpaka nyumbani wakirudi kule baba yao alikwenda kutembea tena njaa. « Ingieni ndani sasa tuandikishe mali tule ». Akiingia ndani : « kachukueni chano ». Wamekwenda kuchukua kule kule, walikoweka kule. Wakija nacho pale. « Chano andika ! » kimya. « Chano andika ! » kimya. Anauliza baba mtu : « chano hiki imekuwaje leo, mboni hivi ? sijui, sijui... wewe mama mtu ulikwenda wapi ? », « nilikwenda nyumba ile nilikwenda kufanyaje », « sasa nyinyi watoto, chano hiki kimekuwaje ? » Watoto wadogo wanasema : « walikuja watoto wa Sultani tulikwenda kukosha kisimani, sasa ndo tukarudi nacho. Basi sijui kuosha huko ndo… », kimenyamaza. « Kuosha wamekuchukulieni wenzenu, sasa leo mtakula nini ? » Hakuna pale cha kusema. « Basi mimi sitafuti tena mtaji, mtapambana nayo njaa mkae hapa mimi natafuta vitu mkae chini nyinyi munawapa watu ».

Basi, siku ile, kutwa, kutwa, njaa imekuja juu. Watoto hawajuani. Baba mtu yule kuchukua tena nsambo wake, mashoka na nini akapite kubangua asali. Akapita kutembea tena ndo kesha kupata mwangaza kusema pale nikienda nitapata tena pale.

Anarudia pale pale, penye mti pale. Akija kapumzika anachukua shoka lake anaanza tena. Bom ! mumjiti mule. « Mtu gani ? sisi tumetoa kitu cha muria kabisa, maisha yako utaishi mpaka leo unakuja tena, wewe au mtu mwingine ? », « ah ! mimi », « wewe kile tulichokukupa umefanyaje ? », « ah ! watoto (wamebadilishiwa) ». Hivi wanasemezana wala hawajui watu walivyokaa ndani mle au kabila gani… « Sasa leo mmekuja kutaka nini tena ? », « sisi hatuna kitu », « ngoja basi. Tutakufanya maarifa. Tena ukipata hiyo maisha utakuwa tajiri moja kwa moja ». Wanatolewa kifimbo, fimbo hii, mkwajuu wanaotembelea wanaume, mzuri ! umetiwa mafuta umefanyaje ? Umepindwa wa kutembelea. Wanamwambia : « kifimbo hicho tunakupa, ukifika nyumbani kwako hata ulivyofanya mwanzo kuanza njiani, uanze ukiwa nyumbani kwako ukaanze, ukaseme : 'kifimbo cheza usicheze na wajinga ucheze na mwerevu kama mimi', basi ndo utajua kitachotoka humu ».

Bwana alidhani kama mwanzo. Akenda pa mjiti hivi uramboni, amekaa : « kifimbo cheza ! usicheze na wajinga, ucheze na mwerevu kama mimi ». Mmm... ! ikiwa kifimbo kinampiga mwenyewe, sasa yule anaruka ruka, analia analia ! « Jamaani mwee ! mimi sifanyi tena ». Anaosema nao wako mbali : « jamaani sifanyi tena, tafadhali ! ». Anachapwa humu, anachapwa humu, anachapwa humu… mpaka kule kule wanatoa sauti : « basi ! » Eh ! ndo kinaanguka bo ! kifimbo kile ! anaokota, anasema : « ah ! mimi leo ngoja nikawarabu watoto walionifanyia mambo haya ».

Anachukua mkwajuu wake na shoka lake, akenda akawakuta kimya. Wamelala njaa akiingia ndani : « nini hapa ? ule ule ! toka juzi si jeuri zao kinapatikana kitu hapa wanafanya mchezo. Basi fungeni mlango kwanza ». Anawaambia : « fungeni mlango kwanza ndo tufanye maarifa ». Akifunga mlango, akiwaamsha wote wamezunguka watoto, anasema : « kifimbo cheza na wajinga na mwerevu kama jamaa hawa, werevu kabisa ». Watoto wanalizana, wanaingia uvunguni sivyo, kwenda chumbani sivyo, wote kama vimegawanyishwa, kama kila mmoja na chake… « We baba tumekoma ! chano kile tulitoa sisi tukawapa watoto wa Sultani kwa hivo baba, tumekoma tafadhali ». Wanasikitika taabaan kule kule mpaka itoke sauti kule : « basi eh ! », bom... kifimbo kile ! (watoto wako) pese pese, madonda matupu ! kufanyaje, kula bado hakujapatikana.

Haya, sasa amekaa ameingia msalani kwenda kukoga maji, baba mtu yule jua tena alasiri. Kavaa nguo zake, kanzu yake, kofia yake, nzuri...."


Inaendelea hapo chini :

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni