04/10/2013

NDOVU

Kila mwaka hapa Tanzania ndovu 10 000 (30 kila siku) wanauawa kinyume na sheria za kidunia. Kwa kuwa wamebaki 40 000, ina maana kwamba baada ya miaka minne au mitano, ndovu wa Tanzania wote watakuwa wamepotea kabisa. Kwa sababu Tanzania ni nchi huru, hatuwezi kuichukulia hoja hii kuwa ni jambo baya. Ni kitendo ambacho viongozi pamoja na wananchi ama hawajali ama wamekipanga kitekelezwe. Watoto wa tanzania ambao hawataona ndovu hata mmoja katika maisha yao ya mbele wasije wakasema baadaye kwamba nchi hii imelaanika. Hapana, kauli hii haikubaliki. Tanzania ina bendera yake, stempu zake na sasa bunduki zake. Nani kasema kwamba nchi hii haiendelei ?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni