23/11/2013

Siasa ya… ndovu


Hapa Tanzania tumebahatika sana kuwa na weledi wengi wenye busara kupindukia, wasayansi wa kibayolojia wengi mno, wataalamu waliobobea sana katika kusoma mazingira ya kiasili, wana vyuoni na maprofesa wanaohimiza wanafunzi wao kila kukicha kutathmini taathira ya maendeleo endelevu juu ya mazingira ya hapa na pale, mbali na wataalamu na galacha wengine waliojikita katika kupima upeo wa bayoanuai katika mawanda mbali mbali kama vile uhai wa vidudu vya msitu asiliya, makabila ya reptilia na vipepeo wa kiendemiki, na kadhalika. Sekta hizi za elimu na sayansi hazina fedha, ndiyo, ndio maana watu hawa wanavutiwa sana nazo, kwa kujitolea ! Hawa wanastahili kupongezwa. Katika muktadha hii, si jambo la kiajabu kuona kwamba mada na maongezi ya kawaida, hususan kabumbu na siasa, zinapuuzwa sana kiasi cha kutuachia katika hali ya bumbuazi. Je, kweli ndovu wale wa Chadema na CCM wamepotea ? au ?

Kwa wasomi hawa, naomba ruhusa ya kuking’oli hapa baadhi ya tovuti ambazo zinazumgumzia hali halisi ya ndovu wa hapa na pale — wanyama hawa — jinsi watakavyopotea kama aiskrimu mikononi mwa mtoto wa kigogo, na hilo si ramli wala raguza bali ni tazamio la kisayansi !




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni