15/12/2014

Ufaransa imepata tuzo ya Nobel katika fasihi… tena !
Ufaransa ni nchi ya fasihi. Kauli hiyo si maoni yangu bali imethibitishwa tena hivi karibuni wakati ambapo nchi hiyo imejaaliwa kupata tuzo nyingine ya Nobel. Tangu Nobel ilipoanzishwa mwaka 1901, Ufaransa imepata si chini ya tuzo 15 katika fasihi, jambo ambalo linadhihirisha wazi kwamba fasihi ni fani mojawapo muhimu katika ukuaji na uendelezaji wa nchi hiyo. Miongoni mwa waliotuzwa sina budi kutaja Henri Bergson (1927), Albert Camus (1957), Jean-Marie Gustave Le Clézio (2008) na Patrick Modiano (2014) mwaka huu. Kwa tuzo hiyo ya mwisho, Ufaransa imepata nafasi ya kwanza katika nchi zote zilizotuzwa zawadi hiyo tangu 1901.
Hakuna maoni:

Chapisha Maoni