28/03/2015

Nimetafsiri mchezo wa kuigiza wa Molière

(…)
SGANARELLE — Mke wangu, tungamana kwanza chonde chonde ! 
MARTINE  — Ukorofi wako nitauvumilia mpaka lini  ? Unafikiri ukorofi na uhuni wako…
SGANARELLE  — Wee tusije juu mke wangu  ! 
MARTINE — Unataka nifanyeje ili utimize wajibu wako ? 
SGANARELLE — Mke wangu, unajua uvumilivu wangu una kikomo chake nao hauchelewi kukatika sasa hivi. 
MARTINE — Sijali sitishiki mie wala usinibabaishe na maneno yako.
SGANARELLE — Mke wangu, kifaa changu, umechemka sasa kama kawaida yako, haya…
MARTINE — Ngoja…mimi sikuogopi wala nini.
SGANARELLE — Habibi naona unataka kupigwa sasa ! 
(…)


Mganga asiyejijua ni mchezo wa kuchekesha ulioandikwa mwaka 1666 na Molière, msanii Mfaransa aliyezaliwa mwaka 1622. Ni tamthilia ya nathari iliyogawika katika maonyesho matatu na sehemu 21. Onyesho la kwanza linatuingiza katika ugomvi baina na Sganarelle na mkewe Martine. Mume anapiga mkewe kisha mkewe anapanga mpango wa kulipiza kisasi. Bighairi ya vituko na vioja vingi vya kutufurahisha, ni tamthilia ambayo inatulazimisha pia tuyatafakari upya maswala mengi yanayotukabili katika maisha yetu : uongo na ukweli, dhuluma na haki, uuke na udume, ujanja na udanganyifu na hasa utumiaji wa lugha iliyokogwa na ulaghai na uzandiki kama ile ya waganga na wasomi wengine wa hoja mbalimbali.

Mchezo huo unauzwa hapa kwenye Amazon :


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni