05/09/2015

Barua kwa ajili ya Waafrika ambao hawajakimbilia Ulaya


« Kwa barua hii, natoa wito mkubwa wa dhati ili vijana wote wa Bongo, walalahoi kwa wachimba chumvi, pamoja na wengine wasiokuwa na kazi — najua kwamba wengi katika washkaji wenzangu muko juu ya mawe — msikawie kuondoka na kufukuzia Ulaya. Dau la mnyonge litakwenda joshi. Wazungu wako tayari sasa kuacha kila kitu. Bamba tayari, jahazi imezibuka, lori imepigwa dafrau, walami mahututi, dripu zimewaishia, chini kokono kokono ! Nendeni basi, chapu chapu, hamna noma, mtapitishwa tu — seng’enge zimeondoshwa — hata kama hamna paspoti. Ulaya siku hizi imetoa pingamizi zote. Na kwa sababu nyinyi ni wathiriwa — na hata kama hamjaonewa, zingatieni kwamba wazungu hupenda maonevu uonevu —, mna haki ya kudai na kudoea chochote kile cha kukusaidieni kimaisha. Sheria zipo, hasa mkitokwa na machozi. Mfano, mkifika huko, kwanza mkapige hema kwenye uwanja panapo Umeya. Kisha mnyoshe mkono. Mtapewa angalau yuro 500 kwanza — « Oya mlami, nisusie yurooo zangu ! » huku mkijifanya mnalia. Na endapo hamjaambua hapo, msijali, tulieni. Kuna NGO nyingi ambazo zitakusaidieni. Mnajua mzungu moyo wake wa bua. Aidha msisahau kutukana, maana mzungu akitukanwa ana tabia ya kujirudi papo kwa papo, mshipa ukimpiga duh, kwani majuto yamemjaa kutokana na hisia zake za kijinga za kuhurumia kila mja mwenye kusononeka (hata mbwa).

Mie yote hayo yananifurahisha mno, roho yangu kwatu, nimefurahi kwa sababu nchi za Ulaya — na katika hizo Ufaransa na Ujerumani ndizo zenye muziki mnene — zitakuja kusambaratika vibaya kutokana na mikondo mikubwa ya wahamiaji wanaopwelewa kila siku kwenye fukwe za Ulaya. Lakini bado ! Kabla ya hapo jamaani, muwahi kwanza, tafadhali msichelewe, mukasevu msije mkajikute katika jopo la muflisi, kwani sasa hakuna mwaliko, uvamiaji tu, mkapate chenu mapema ! Safari hii kweli mtakula uroda kishenzi, kutesa tu, vitu lwaa, mali chekwaa ! Ulaya ? Mchezo tu.

Msisahau msemo wangu : raha ya maovu, aisee !

Hivyo mkaishie kwa Mamtoni mkajiachie huko ! Mambo ya kitishi !

Wa Salaam. »

La nyongeza hapo, huyo mshkaji akitoa mapendekezo yake kuhusu Ulaya na jinsi ya kufika huko :

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni