09/10/2015

Kweli mnataka tusome ?


Si rahisi kukuta tungo ya kifasihi kwa kiswahili inayochekesha. Hawa waandishi wa EAfC (East African literature Community ?) wote ni watu siriasi kabisa. Wamechemka kishenzi yaani — hapo msomaji tayari keshanikimbia (afadhali hivyo, kwani mimi mzungu, unajua wazungu hawana neno hilo « ashakum » katika lugha yao, halafu utamaduni wao, si unajua ulivyo...). Si jambo la kushangaza kuona kwamba wakina buraza wa vijiweni wako damdam katika kutema kibongo kuliko kumaindi kubukua. Maybe inategemea context yake (hapo msomaji amerudi kwa kuwa naonyesha wazi kwamba nimeelimika (si ngeli inapanda ?) kwani most of them (sasa nimependwa sana, subiri kidogo, hapo nitataja Magufuli) wamevuliwa makofi na wanene wa Mlimani. Kwani ndo hao wakina broo wanaotema mafinyufinyu ya kuleta ucheshi kibao, hata mzuka hatembei tena. Mfano ukipiga tochi hapo mtoto chakalamu jinsi anavyowashusha wale mababu makubwa wa Univasitiz, unafikiri mwandishi wa dizim ana uwezo wa kumsebeza wakina mshkaji, kweli ? Thubutu !

Hapo napoishi Kampala, leo hii nimekwenda katika bookshopi ya mjini. Hiyo inaitwa Aristoc. Wala sikujua kwamba Aristotile ametalii (au twalii ?) kanda hiyo ya « lulu ya Afrika » mpaka kubwaga kirago chake miongoni wa mabantu wa Victoria. Nikaingia ndani, angalau nipate kumwaga macho tu, au kwa maneno ya kiunguja, nitie macho nuru. Basi hapo ndipo nikagundua kwamba Waganda wamefaidi kinoma kwa kwenda mbele sana. Yaani humo humo, ndani ya bukushopi, mtu anajichana buku za kimombo si mchezo. Rafu zote zimesheheni kila aina ya buku, na vyote katika lugha ya kikoloni, raha mustarehe aisee. Mtu anafaidi kikweli. Lakini mie machale yamenicheza, kumbe watanzania wamejichanganya vibaya na wamenihadaa mimi mzungu ! Kwani nilitaka sijui manoveli ya kiswahili, lakini nikayatafuta — unajua mzungu kazinza kichwa — hadi nikachoka. Nikamwendea msaidizi anitilie pondo akanionyeshee sekta ya kiswahili. Kiswahili ? Wewe mzungu wa reli unataka sisi tuingie katika biashara ya patapotea ? Afadhali kazi ya kijungu meko au hizo za kutoboa vidole, si unajua zile za kushonea kofia ya kibongo, « haya durufu darizi babu » ! Basi ikawa katuni kubwa hata Prof Juha bin Boga wa Jiunivasitiz wa Bongo angerudi madarasani kubonga ung’eng’e. Na vipo, yes, kama kumi hivi, vile duni vilivyochanika chanika ambavyo hata mbanyani wa Kariakoo asingekubali kuviuza. Ama kweli mchambia mgomba huondoka na mavi yake !

                          

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni