17/10/2015

Wizi wa makala yangu !

Leo nimekuta makala yangu inayoitwa "Historia fupi ya Kilwa katika maandishi" niliyoandika zamani kidogo kuhusu Kilwa hapo hapo penye JamiiForum. Mwanablogu anayeitwa au ambaye amejipachika jina la MziziMkavu ameniibia makala hiyo bila hata kunitaja. Je nauliza, kweli kitendo kama hicho ni cha ustaarabu ? Najua kwamba mimi ni mzungu, na pengine kwa sababu hiyo, nastahili kudharauliwa. Najua pia kwamba Tanzania kibaka akiiba chungwa sokoni anauawa mara moja. Hiyo ndiyo sheria ya Tanzania. Kwa hivyo hapo nifanye nini ?Hakuna maoni:

Chapisha Maoni