23/11/2015

Uandishi wa habari unavyogeuka ujinga


Leo hii nimesoma makala ya kijinga kutoka katika gazeti ya The East African (novemba 21-27-2015). Makala hiyo inazungumzia uhayawani wa kiislamu uliofanyika hivi karibuni Ufaransa. Mwandishi huyo, ambaye jina lake silitaji hapo, anadai kwamba Ufaransa imevamiwa kwa sababu ni nchi yenye ubaguzi na ugozi. Nadhani huyo mwandishi anaonyesha wazi kwamba hana akili ; na nikisema hivyo si kwa sababu amechafua nchi nilikozaliwa (sisi Wafaransa tumezoea sana ukosoaji) bali nazidi kushangaa kila siku kuona jinsi mtu mwenye ujuzi fulani anavyoweza kuwa mpumbavu kiasi hicho. Je, nchi zile zote, na ni nyingi mno sasa — msomaji bonyeza HAPA —, ambazo zimepigwa na ubedui na ushenzi huo usiokuwa na mfano, je zimevamiwa kwa sababu hizo ? Na Tanzania ilipolipuliwa kwenye Ubalozi wa Marekani mwaka 1998, ni kwa sababu ya ugozi uliopo katika nchi hiyo (dhidi ya maalbino) ? Ama kweli dunia yetu ni ya kuchukizana...

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni