13/06/2016

Tembo "yetu" nusura kuingia mitini ?


Leo nimefurahi sana kuwakuta Watanzania wakipiga kampeni ya kuokoa tembo wa Tanzania. Mimi nilifikiri kwamba swala hilo la kupenda viumbe hai kama wanyama wa porini lilikuwa la kizungu, swala ambalo kwa hivyo ni la kupuuza. Kumbe hata Watanzania wamejitolea katika kutetea "haki" ya tembo. Katika utafiti niliofanya Tanzania kwa miaka zaidi ya 25, sijakuta jamaa mmoja aliyeweza kunijibu swala langu lifuatalo : "kwa nini twiga ana shingo ndefu ?" au jingine hilo "kwa nini punda milia ana milia ?" Basi hadi leo, maswala hayo yanatatanisha vikundi mbalimbali vya wana sayansi duniani kote… isipokuwa Tanzania kunako twiga na punda milia ! Nani anajua kwamba tembo wanawasiliana kwa kutumia miguu yao hata kama wameachana kwa masafa marefu ? Laiti watoto wa Tanzania wangejua mambo hayo, nadhani wangekuwa wapenzi wa kweli wa wanyama hawa pamoja na wengine wa kiajabu. Kwa maneno machache, wangekuwa ni wazalendo na wapenzi wa nchi yao. Lakini watu wazima wenye ujuzi huo na wazee wenye hekima na busara wako wapi ? 


Jinsi Hifadhi ya Selous ilivyouzwa : RIPOTI HAPA

https://www.facebook.com/OKOATemboWaTanzania

http://wwf.panda.org/wwf_news/?269211/elephants-could-disappear-from-tanzania-world-heritage-site-within-six-years

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni