11/08/2016

Sarah Waiswa amepata tuzo la Arles


Sarah Waiswa amepata tuzo la Arles (Ufaransa) katika usanii wa picha mwaka 2016. Ni tuzo ambalo linatolewa kila mwaka ili kuhamasisha na kuimarisha usanii bora katika uwanja wa picha. Sarah Waiswa ametunukiwa tuzo hili ("Discovery Award") kwa sababu ya kazi yake juu ya Mazeruzeru (maalbino kwa kiswahili chenye « siasa bora ») ambao huuawa kila mwaka na viungo vyao vya mwili kuuzwa kutokana na itikadi za kishenzi ambazo zimeshamiri sana miaka hii Afrika mashariki. Sarah Waiswa ni mzaliwa wa Kenya ingawa ni raia wa Uganda na picha zake (« Stranger in familiar land ») zilionyeshwa katika tamasha ya Arles hivi karibuni. Wasomaji ambao wanapenda ubunifu kama mimi wanatakiwa kufuata anwani hizi zifuatazo :

ARLES

SARAH WAISWA 

Courtesy@Sarah Waiswa
Courtesy@Sarah WaiswaHakuna maoni:

Chapisha Maoni