04/09/2016

UKUNI MBAYA HAUFICHIKI


Nimetunga mchezo wa kuigiza uitwao "Ukuni mbaya haufichiki" ambao unapatikana katika mtandao wa Amazon (hapa). Ifuatayo ni muhtasari wake :

Profesa Buruji anajulikana dunia nzima kwa sifa zake katika kupambana na ukoloni mambo leo. Lakini leo amechanganyikiwa. Majojo yamemzonga. Licha ya rushwa alizozipokea na mgongano wa maslahi uliomkashifu, mwanawe Halima amemjia na habari mbaya. Amepata mimba kabla ya ndoa. Mama yake ndiye atakayemtetea, kwa harija na jazba, ili mumewe asimpeleke mwanao kijijini. Ugomvi na zogo zikatokea hadi kutoelewana kukakithiri na kuleta mfarakano mkubwa. Mambo yangezidi kuwa mabaya na talaka ingeandikwa papo hapo kama si mgeni kujitokeza. Na itakuwaje mgeni huyo awe Mmarekani ambaye ajitambulishe ni ndugu yake pacha ya Halima ? Kitandawili hiki, pamoja na kwamba kinaingiza mshangao mkubwa katika familia ya Prof Buruji, ndicho kinacholeta habari ya kiajabu, kiasi cha kutibua siri zote za zamani na kutetemesha familia nzima. Ndipo inafahamika kwamba nyuma ya mgogoro huo kuna jambo la msingi ambalo binadamu anapaswa kulitilia maanani, jambo ambalo ni upendo.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni