14/03/2018

Nimetunga mchezo wa kuigiza


Katika mchezo huu wa kuigiza, tuko katika Ufalme wa kufikirika. Wahusika, ambao ni sanamu, wamekusanyika katika dunia ambayo imeangamia. Mazingira yamefikwa na uchafu, misitu imekatwa, maziwa na mito zimejaa takataka, maji ya bahari ni mmumunyo wa plastiki, miji mikubwa imezingirwa na moshi mweusi mkali, nyika zimeondokewa na dalili zote za uhai, na kadhalika. Juu ya hayo yote, spishi zote za wanyama zimepotea. Mazingira yabisi, ardhi kame, udongo tasa, yai viza ; binadamu mwenye tamaa na husuda.

Kumetokezea nini hata binadamu hawezi kukitegua kitandawili hiki kinachomzunguka ? Hapo hakuna mji hadi msomaji akubali kutembea kisengesenge katika dunia ya kisaasili ; kile ambacho kilicholetwa na baadhi ya wanyamapori, zamani ya kale. Wao ndio wanaojitahidi, katika mchezo huo huzuni, kujibu swali hilo zito : kwa nini ?

Hiyo ndiyo tamthilia ambayo imetungwa kishairi. Mashairi yote — mashairi ya mapokeo, maguni, masivina na mashairi huru — yanaghaniwa na wanyamapori waliopotea kabisa. Sauti yao, kupitia koma zao, ndiyo itakayorindima katika akili zetu chakavu ambazo zimetekwa na dhana ya kibaada-ya-ustaarabu.Ili kupakua kitabu hiki, tafadhali bofya kwenye picha ya juu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni