12/07/2018

Nimetunga mchezo wa kuigiza


                                


Tamthiliya hii ni ya mhusika mmoja ambaye amelazwa hospitali. Hali yake si mbaya sana ingawa amefungwa bendeji na kata mwili mzima. Macho yake pekee ndiyo yanayoonekana. Na bila shaka msikilizaji utapenda kujua ni nani anayejificha ndani ya deraya hiyo ya bendeji. Itabidi umsikilize anavyojisemea. Na kwa kuwa yuko peke yake, anaongea na nafsi yake, mara Biti Nadhiri, mara Ndugu Akili, mara dada Hemko. Mjomba Utani pia hutokezea mara kwa mara. Huenda utakisi ni mzungu ikiwa utahisi kuwa fani zake zinadhihirisha mkabala wa kitiishi. Mzungu si mbabe mbabe ? Lakini mbona mhusika huyo anaonekana hana nadhari kubwa wakati anashindwa kuwa mtambuzi aliyekomaa ? Si mantiki imemezwa na jabza ? Hapo huenda hadhira itabaini kwamba imekutana na Mwafrika. Mwafrika si hajijui ? Lakini Mwafrika hawezi kufanana na Mzungu. La hasha. Hivyo huyo mlazwa ni nani ? Kitandawili hiki utastahimili nacho hadi mwisho wa mchezo huo wa kuigiza. Na katika dunia yetu ya kuchukizana, dunia ya kila mtu na simu yake, kujua wapi na katika kabila gani mtu anakotoka si hoja chapwa. Au pengine kipindi tulicho nacho sasa hivi kimekuwa kipindi kipya, kile cha kuzalisha kizazi kipya, ambacho bila shaka hakina kipya ? Je, inawezekana kuwa binadamu amezuka Adamu shume, asiyekuwa na asili wala ngozi ?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni